Mambo 3 Muhimu ya Kuzingatia kwenye maisha
Katika maisha ya mwanadamu
Yapo Mambo mengi ambayo huvuta umakini wa Kila mtu,Miongoni mwa Mambo hayo yapo Mambo matatu ambayo kutokana na takwimu za utafiti nilioufanya yameshika na kukamata hatamu ya umakini wa maisha ya mwanadamu.
Mambo haya matatu yamepelekea kuwepo na matapeli wengi Sana katika nchi mbalimbali Tena Mambo haya yameongeza udanganyifu mkubwa katika maisha.
Mambo haya matatu kila ukipita katika maeneo mbalimbali mjini utakutana na vibao vinavyotaja kuhudumia watu katika Mambo hayo.
Tena wametokea wachungaji na wahubiri wengi wakiyapa kipaumbele Mambo haya kwa sababu ndio yanagusa maisha ya mwanadamu kwa asilimia zaidi ya 90%.Zaidi wakaibuka mitume na manabii wa Kila Aina wakifungua makanisa yao na kuwahubiria watu juu ya Mambo haya matatu.
Katika haya Mambo matatu watu wengi wamejiingiza katika dhambi na kumkana Mungu katika kuyatafuta.Leo nataka tuyazungumzie kwa undani Sana ili tujue namna ya kuyatafuta kwa njia halali huku Tukimtumikia Mungu.
Mambo hayo ni
(1)MAFANIKIO(Achievement)
(2)UMAARUFU(Popularity)
(3)UPENDO (Love)
(1) MAFANIKIO
Maneno ya Mungu yanasema tujitabirie makubwa na ushindi na wengi huwa tunawaza mafanikio tu.Mungu alituumba ili tuwe washindi.Utafiti unaonyesha kuwa asilimia kubwa ya watu duniani wanapenda kufanikiwa na Wana malengo ya kufika mbali ingawaje watu wanao ambatana nao ndio wanao wakwamisha wasifike mahali walipoumbiwa kuwa kwa wakati.
Wamejitokeza waganga wa kienyeji wakizungumzia suala la mafanikio na wakiahidi kumpa mtu mafanikio pindi atakapofuata matakwa yao.Ni kweli unaweza ukafanikiwa kupitia watu Hawa lakini Mafanikio yao ni ya majuto na ni ya muda tu,Mafanikio ya kweli yanatoka kwa Mungu.
Leo nataka nikuambie wengi huwa wana laghaiwa kwa kutumia sehemu hii ya mafanikio katika Maisha.Watajitokeza watu wa namna mbalimbali ili kukuvuta katika njia mbalimbali za mafanikio lakini kabla haujaingia katika njia hizo hebu jipime katika sifa nne za watu wenye kufanikiwa katika maisha;
(1)Watu wanaofanikiwa siku zote huwa na hamu ya kufanikiwa zaidi ya wengine hivyo kuweka juhudi kubwa katika kazi.
(2)Ni watu wanaopenda matokeo ya mafanikio yao yawe yametokana na jitihada zao na Mungu wao
(3)Ni watu wanaosonga mbele aidha wamefanikiwa au hawajafanikiwa,Aidha wamekubaliwa au wamekataliwa,Wana Imani kubwa katika neno “siku moja nitashinda”
(4)Ni watu wanaopenda kuanza na kazi ngumu Kwanza Kisha kumaliza na zile nyepesi,Huwa na vipaumbele makini Sana katika maisha yao.
Kuna namna zitakuja kwa uzuri na ubora kabisa lakini ndani yake zimejaa dhambi Cha kufanya ni kuwa makini(beautiful package with sinfully content)
(2)Umaarufu
Jambo lingine ambalo limekamata watu wengi ni umaarufu.Watu wa kila Aina wamekuwa wakitafuta umaarufu kwa njia mbalimbali,Wengine wameamua mpaka kumwabudu shetani ili tu wawe watu maarufu na tunawajua,Wengine wameamua kuwa waasherati wa viwango vya lami ili tu wajulikane na watu,wengine wamejidhalilisha na kukaa Hadi utupu mbele za watu ili wawe maarufu na wengine wamejitoa miili yao ikatumiwa na watu ambao waliwaahidi kuwashika mkono ili wawe maarufu.
Watu wanaotumia nguvu zote ili kuwa maarufu huku wakimwacha Mungu huishia mahala pasipofaa maana ujira wao wanakuwa wameshaupata.
Zipo njia nne za kukuza brand yako lakini sio kwa kufanya Mambo yaliyo kinyume na Mungu aliye juu(somo lingine).
(3)UPENDO/mapenzi
Kila ukipita mitaani utakutana na mabango ya waganga wa kienyeji yanayotangaza kutoa huduma za kukuza uchumi,kurudisha wapenzi,kufanya mtu awe maarufu.Wengine ni manabii na mitume nao wamejikita katika Mambo hayo hayo na wanavutia watu wengi mnooo, Vyombo vya habari na runinga vituo mbali mbali vya utangazaji asilimia kubwa ya vipindi vyao ni vyenye mada hizo tu.hapa ndipo utagundua kwamba mwanadamu wa leo amekamatwa Sana na haya mambo matatu.
Wengi ambao wamekurupuka kutafuta mteremko katika Mambo haya wameishia kujiingiza katika uasherati,uchawi na zinaa na kushindwa kupata thamani stahiki waliyoumbwa wawe nayo.
Wakati unapofikiria kuvitafuta vitu hivyo vitatu kuwa makini Sana maana Kuna mazingira yatakuja kwa uzuri kabisa lakini usipokuwa makini yatakuangusha na kukufanya ushindwe kufika mahali ulipopaswa ufike.
Umakini unahitajika Sana,
Najua unahitaji kufika mbali Sana,Mungu akusimamie ufike mahali unapostahili ufike.Ubarikiwe Sana!
Kupata vitabu vyangu jitahidi uwatafute
MAWAKALA TANZANIA ????????
Iringa
0755100502
0753-690907
Au tembelea Citymax Booshop!
Dodoma
0755100503
0753 690 907
Au tembelea Citymax Booshop!
Tabora
0765052507
Tanga
0627186623
Biharamulo
0753383461
Mtwara
0786408811 au 0717408811
Dar es Salaam
0745252670 au 0756094875
Mbeya
0744241744
Mbeya Mwanjelwa 0763943695
Kahama
0767872191 au 0657948776
Tunduma
0685453333
0769634248
0656512333
Katavi
0762255463
Moshi na Arusha
0744 126 082
Morogoro
0782144920
Kahama
0755833533
Dodoma mjini Mipango
0692983162
Makambako
0762282599
0674246969
Au tembelea P. M Stationery and Book Shop Makambako Mizani
Mwanza
0754 977 848, Lavena
Mwanza mjini
0767949399/0652707919
Mikumi Morogoro
0757010979
0715010979
Singida na Katesh-Babati
0789457475
Dar es Salaam Temeke yombo
0672046203/ 0746270942
Kariakoo
0783948848
Moshi MJINI
0624873870/ 0752250938
Kwa mlioko nje ya nchi tunatuma kwa DHL, piga namba 0753-690907
Unataka uwakala? Piga 0753-690907
@yurisdutch
yurisdutch@gmail.com