Usikate Tamaa

Usikate Tamaa

Wakati Fulani katika maisha Kuna Hali napenda kuiita family poverty cycle,kipindi kisicho na mafanikio kwa familia nzima au ukoo mzima. Yaani unakuta familia nzima au ukoo mzima wanapambana Sana lakini hakuna mtu hata mmoja katika ukoo au familia anayevunja wigo wa mafanikio ambao umekuwepo.

Kama walikuwa ni masikini Basi wanaendelea kuwa masikini vilevile mpaka asubuhi, Kama ukoo ulikuwa wa watu dhaifu Basi mnaendelea kuwa dhaifu mpaka asubuhi. Kama walikuwa wanasumbuliwa na magonjwa Basi mwendo unakuwa huohuo miaka na miaka.

Hii Hali ni Hali isiyovumilika na ambayo haipaswi kuvuliwa hata kidogo maana Ina tabia ya kuaminisha na kuhitimisha udhaifu wa familia miaka nenda Rudi.

Kama ukoo ulikuwa wa kimasikini Basi umasikini utaendelea kuuwinda ukoo au familia hio mpaka kieleweke,ni Kama laana hivi,,

Utasikia ; hao huwa wakijitahidi Sana Basi wanapata mtoto anayekuwa mwalimu, hao wakijitahidi Sana, wanakuwa na kijana atakayekuwa mtendaji.

Kila wakipambana wanaishia kuwa watu wenye thamanj ya chini ukilinganisha na familia nyingine zenye background sawa na hii. Yaani familia inakuwa ya kawaida hata Kama wanafamilia wanajitihada kwa kiasi gani.

Kila wakipambana Basi wanaishia katika level ya chini kabisa ya mafanikio. Na watu wanakuwa wamewazoea kuwepo katika level hizo za chini.

Hii ni Hali inayotesa jamii nyingi Sana za watu duniani na huenda wewe ni mmoja wa watu waliopo katika mizunguko ya namna hii na watu tayari wameshahitimisha kwamba hata ufanye Nini hauwezi kuvunja wigo wa mzunguko huu na utaendelea kuwa masikini.

Leo hii nataka nikuambie kitu muhimu Sana ,kitu ambacho ukikizingatia utavunja wigo huu uliowekwa na Imani za watu juu ya mafanikio yako na ukoo au familia yako.

Kitu Cha Kwanza kabisa na Cha muhimu mno unachotakiwa kufanya ni kuamini kwamba unaweza kuvunja wigo huu, Imani yako ya ndani ndio nguvu ya Kwanza kabisa katika kuvunja wigo huu.

Kitu chochote kikubwa na chenye maana katika maisha ya mtu lazima kianzie ndani. Kwa hiyo kitu cha Kwanza lazima uamini kwamba unaweza kuvunja wigo huu uliojengwa na Imani za watu juu ya mafanikio yako na familia yenu kiujumla.

Kitu kingine unachotakiwa kujua ni kuwa, lazima ukutane na strangers, watu ambao hamfahamiani na ndio watu ambao watabadili maisha yako mazima. Kwa lugha nyingine lazima uwe tayari kupokea watu wapya katika maisha yako ili uweze kuvunja wigo huu. Lazima ukubali kuwa na urafiki na watu wengine wenye uwezo kuliko wewe.

Yule mwizi pale msalabani alikutana na Stranger ambaye ni Yesu ambaye alibadili Maisha yake mazima, Mzee Mengi alikutana na strangers ambao walibadili maisha yake mazima, Mpagaze unaomuona na kumsikia Leo alikutana na strangers na ndio akaamka alipokuwa , Wakina Joel Nanauka wote Hawa walikutana na strangers na hao wakawasaidia kuvunja ule wigo ambao jamii huwa inauweka katika maisha ya familia zetu,

Hawa strangers sio watu wa familia moja na wewe Bali ni watu walio nje ya mzunguko unaowakabili.

Wewe pia lazima ukutane na watu tofauti na ulionao Sasa ili uvunje ukuta huu nisioupenda.Kumbuka mvunjaji wa ukuta huu utakuwa ni wewe hao strangers watakusaidia tu kukutengenezea mazingira lakini muhusika mkuu ni wewe wapo unayesoma hapa. Wewe unaesoma ndio muhusika ninayemzungumzia.

Hakuna chochote kinachoweza kushindikana Kama utaamua kwelikweli kuivalia njuga Hali hii ya aibu.

Family poverty cycle itatengenezea watu mitazamo ya kushindwa juu ya familia yenu lakini Imani thabiti kwa Mungu aluye juu na kujituma kwako kunaweza kuvunja wigo huu kwa uhakika.

Watu wote ambao walichukizwa na cycle hii na kuamua kupambana nayo walifanikiwa, hata wewe hapo unaweza kuvunja wigo huu, Usiogope, Kila kitu kitapatikana ukiwa safarini, Anza kupambana Sasa hivi.

Kwa jinsi ninavyoichukia Hali hii ,naendelea kumuombea Kila aliye katika mfumo wa mizunguko hii ya kushindwa na kutofanikiwa ikashindwe kwa jina la Yesu kristo.

Mungu akusaidie uvunje wigo huu mbaya ili kuipa ahueni familia yenu na kuiondoa kabisa katika umasikini na mateso ya Imani za watu.

Dear friends

God bless you so much

Kupata kitabu Cha wewe ni Nani bofya hapa https://www.getvalue.co/prod/wewe_ni_nani__1
@yurisdutch
Professor
Contacts
yurisdutch@gmail.com
0768969596