Wake Up Call
Kuna mambo mengi Sana unatakiwa uyafanye ili kutimiza Kusudi la kuumbwa kwako bro, Mungu tayari alikwisha kupa thamani kubwa na ipo ndani yako Cha msingi Ni wewe kuijua ili kuishi katika viwango vya juu vya thamani alivyokupangia uviishi,
Cha ajabu na Cha kushangaza pamoja na kuumbwa na thamani kubwa ndani yao, Kuna watu wanaishi katika viwango vya chini Sana vya thamani.
Utakuta wale walioumbwa waishi Kama Wana na binti za kifalme wanaishi kama watumwa na ombaomba.
Wale waliopewa mavazi Safi na ya thamani wanayatupa na kujipaka matope katika miili yao.
Mungu alikukaribisha katika ufalme wake ili uiishi maisha ya kifalme Lakini wewe ukaamua uende mbali na ufalme na ulipofika huko ulipokwenda ukaanza kuishi maisha ya utumwa, huoni Kuna haja ya kurudi nyumbani??
Umeacha vinono vingi na kila thamani uitakayo yenye Neema ambayo IPO ndani ya nyumba ya baba yako, huko uliko Ni shida tupu, Rudi nyumbani.
Kusudi Ni kiti Cha enzi Cha mwanadamu duniani (WEWE NI NANI by Yuris Dutch). Sehemu yako ya utawala unaiacha iangamie na kwenda kushikilia mahali panapokutawala. Badala ya kuwa kiongozi wewe ndio unaanza kuongozwa. Fikiria Mara mbili na uchukue maamuzi.
@yurisdutch
yurisdutch@gmail.com